Habari
DKT. JAFO ASHIRIKI KONGAMANO LA MAJADILIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI 2024.

DKT. JAFO ASHIRIKI KONGAMANO LA MAJADILIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI 2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameshiriki Ufunguzi wa Kongamano la Mwaka la Majadiliano ya Biashara na Uwekezaji kati ya Serikali na Sekta binafsi 2024 pamoja na Mkutano Mkuu wa 49 wa Mwaka 2024 wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Disemba 06,2024. Katika Ukumbi wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Katika Kongamano hilo Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb).