Habari
DKT. JAFO ASHIRIKI ZOEZI LA KUPANDA MITI KIBAHA,PWANI.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) akipanda Mti katika shule ya Sekondari Bundikani kabla ya kufunguzi rasmi Maonesho ya Biashara na Uwekezaji yanayofanyika katika Viwanja vya Maili Moja Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Desemba 17,2024..
Aidha Dkt.Jafo ametoa rai kwa Wawekezaji wa Viwanda Nchini wanapoendelea na shuguli za Uwekezaji na Uzalishaji kuendelea kutunza Mazingira na Kupanda miti kwa wingi ili kuunga Mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu ya kutunza Mazingira pamoja na Matumizi ya Nishati safi.