Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI KAPINGA AIAGIZA TANTRADE KUKUZA BIASHARA KWA KASI NA WELEDI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga ameiagiza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), kufanya kazi kwa kasi, weledi na ushirikiano ili kukuza uchumi wa Watanzania kwa ujumla.

Ameyasema hayo Novemba 28, 2025 jijini Dar es Salaam alipotembelea Mamlaka hiyo, akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Dkt Suleiman Serera pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Bw. Sempeho Manongi, na kuzungumza na Bodi pamoja na Menejimenti ya TANTRADE.

Vilevile, ameisisitiza TANTRADE kuhakikisha mifumo ya TEHAMA inasomana, kurahisisha upatikanaji wa taarifa za masoko kwa kutumia teknolojia rahisi.

Aidha, Waziri Kapinga ameiasa TANTRADE kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pamoja na kuhuisha ya sheria ili ziendane na wakati ikiwa ni hatua ya uboreshaji wa mazingira ya biashara na kuvutia kuvutia ufanyaji biashara na kukuza biashara.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE Prof. Ulingeta Mbamba ameahidi kuwa Mamlaka hiyo iko tayari kutekeleza maagizo hayo ili kukuza biashara kwa maslahi ya nchi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Dkt. Latifa Khamis amesema Mamlaka hiyo itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi kuanzisha Ofisi katika Mikoa mbalimbali hasa mikoa ya mipakani ambayo ni mikoa ya kimkakati kwa TANTRADE.