Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Jafo - Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji Biashara.


DKT.JAFO - SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UFANYAJI BIASHARA.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Suleiman Jafo (Mb) amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa kuweka miundombinu wezeshi kama barabara, umeme wa viwandani, maji , kuondoa tozo na kurekebisha Sheria , Taratibu na Kanuni ambazo ni kero kwa wafanyabiashara.

Ameyasema hayo Februari 19, 2025 wakati akijibu hoja mbalimbali katika Mkutano wake na Wadau wa sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji wa Mkoa wa Njombe uliolenga kusikiliza changamoto walizonazo na kutafuta namna bora ya kuzitatua.

Vilevile amesema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto hizo za kibiashara zikiwemo za matuta mengi barabarani, vizuizi vingi vya mageti, kodi, tozo, ubora wa bidhaa, vipimo sahihi , urasimu wa upatikanaji wa mikopo na Wafanyabiashara wageni kuchukua nafasi za Watanzania kwa kishirikiana na Wizara za kisekta na Taasisi husika ili kuhakikisha wafanyabiashara hao wanafanya biashara kwa tija.

Aidha , ametoa rai kwa Wananchi wa Njombe kuhakikisha wanatunza amani na usalama wakati wa uchaguzi kwa kuwa ndio msingi wa ufanyaji biashara huku akiwataka wafabyabiashara na watumishi wa umma kushirikiana na kufanya kazi kwa upendo.

Dkt Jafo pia amewataka Wafanyabiaahara hao kuchangamkia fursa za masoko ya
ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na hata katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) na Mpango wa Ukuaji na Fursa wa Afrika (AGOA) ili kukuza biashara na uchumi wa nchi.

Naye Mkuu Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa wake utaendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa wafanyabiashara hao okiwemo tozo ambazo ni kero kwa wafanyabiashara hao ili waweze kufanya biashara zao kwa tija.