Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI KAPINGA AZINDUA MTAMBO MPYA WA KISASA SBC (PEPSI)


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga amezindua laini mpya ya pili ya mtambo wa kuzalisha vinywaji wa SBC Tanzania utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha katoni 57,000 kwa siku.

Kapinga ameyasema hayo mara baada ya kuzindua mtambo huo Mei 20, 2026 jijini Dar es Salaam.

Waziri Kapinga amesema kuwa uwekezaji huo umefanya kuwa na ongezeko la mapato ya Serikali, pamoja na kupanua ajira kwa watanzania. Hatua hiyo inakwenda kikamilifu na dira ya Serikali ya kujenga uchumi imara na shindani wa viwanda nchini.

Aidha, Kapinga amefafanua kuwa Serikali imefungua milango na wawekezaji na hatua hiyo inaonesha dhahiri wawekezaji kuwa na imani na kumekuwa na ongezeko la wawekezaji nchini.

"Naipongeza SBC kwa kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla na hii sisi kama Serikali niwahakikishie tutawawekea mazingira rafiki mazuri na wezeshi katika kupanua wigo wa uwekezaji". Kapinga.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SBC, Bw. Ziad El Khalili amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka 25 iliyopita tayari wameshafanya uwekezaji wa Shilingi Bilioni 850 nchini Tanzania. Amefafanua kuwa wanajivunia kuongeza ajira na tayari wameshatoa ajira za moja kwa moja zipatazo 15,000/ na zile ambazo sio za moja kwa moja kwa makundi tofauti.Hata hivyo, upanuaji huo wa kiwanda umejumuisha kuweka miundombinu ya kisasa ya uzalishaji,maghala na miundombinu ya mazingira ya mitambo ya kusafirisha majitaka ya viwanda.