Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. KIjaji awataka Wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya AGOA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu kijaji
(Mb) amewataka wafanyabiashara Nchini kuchangamkia fursa ya Sheria ya ukuaji wa fursa Afrika (AGOA) ili kuweza kupata masoko nje ya Nchi hususani katika Nchi ya Marekani.


Amebainisha hayo Oktoba 30,2023 katika Kikao cha pamoja na wadau wa mpango wa AGOA katika Ukumbi wa Mikutano wa FCC Jijini Dar es Salaam.
Dkt.Kijaji amesema kuwa kama wafanyabiashara hawana budi kwenda sambaba na fursa hiyo ili kuweza kukimbia kwa pamoja katika soko la Bidhaa Duniani kwa kuzingatia ubora wa bidhaa pamoja na uzalishaji wa bidhaa thabiti kwani Soko la Marekani huhitaji bidhaa wakati wote na na sio kwa kusuasua.


Aidha amewataka wafanyabishara hao hasa wale wadogo kuungana kwa pamoja ili kuweza kupata
bidhaa nyingi zaidi kwa pamoja ili kurahisisha usafirishaji vilevile amewataka kujenga tabia ya kushirikiana kwa kutembeleana katika biashara zao ili kujifunza kwa kila mmoja wao.


Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah amesema kuwa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara nii kuhakikisha inaweka Mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wamiliki wa Viwanda katika ufanyaji wa shughuli zao.

Kwa upande wa Washiriki wa Kikao hicho Bi.Jalia Majura kutoka kampuni ya Compete ametoa pongezi kubwa kwa Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuhakikisha Wafanyabiashara nchini wanaifahamu fursa hiyo ya AGOA kwani itaondoa usafirishaji bidhaa wa binafsi na kuwa Usafirishaji wa bidhaa pamoja