Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

DKT. KIJAJI AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA VIWANDA KUJADILI CHANGAMOTO ZAO.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk, Ashatu Kijaji, amekutana na wawekezaji, na wamiliki wa viwanda mbalimbali  na kujadiili changamoto wanazokabiliana nazo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na kujenga uchumi shindani na viwanda.

Katika mikutano hiyo, Waziri Kijaji amekutana na Viongozi wa Kampuni ya Dangote Tanzania inayozalisha Saruji, Kampuni ya Coca - Cola KWANZA LTD inayozalisha bidhaa mbalimbali za vinywaji baridi na Wawekezaji wa Kampuni ya Gynile kutoka Misri inayotarajia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mbolea nchini.

Wakati huo huo, Waziri Kijaji amekutana na baadhi ya Watendaji Wakuu wa Tume ya Ushindani (FCC)

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghala (WRRB ) na  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na  Biashara kujadili utekelezaji wa  majukumu ya Taasisi hizo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla.

Aidha  Waziri Dkt. Kijaji amezitaka taasisi zote chini ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kufanyakazi kwa ushirikikiano na kuepuka kuwa kikwazo kwa wawekezaji, wenye viwanda na wafanyabiashara  ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ili kuendeleza na kukuza sekta ya uwekezaji, viwanda na uchumi.