Habari
Dkt.Selemani Jafo (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Mhe. Ahn Eunju
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Mhe. Ahn Eunju na ujumbe wake katika Ofisi ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam, Novemba 13, 2024.
Ugeni wa Balozi Mhe.Eunju umelenga kujitambulisha tangu alipoteuliwa kuwa balozi nchini pamoja na kufanya Mazungumzo na kujadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.