Habari
MHE. LONDO , WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA KOREA, WAJADILI UIMARISHAJI WA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA BIASHARA
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), amekutana na ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Korea ukiongozwa na Mhe. Joon-Byeong Yoon, Rais wa Kundi la Urafiki wa Wabunge wa Korea na Tanzania, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara nauwekezaji kati ya nchi hizo mbili Juni 12,2026 Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili ziliridhishwana ukuaji wa uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Korea Kusini, ambapo thamani yabiashara baina ya nchi hizo ilifikia Dola za Marekanimilioni 222.84 mwaka 2025.
Mhe. Londo alieleza dhamira ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuharakisha maendeleo ya viwanda na kuongeza thamani ya malighafi zinazozalishwa nchini ambapo Katika hilo, aliikaribisha Korea Kusini kuwekeza zaidi katika viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao na rasilimali za Tanzania ili kuongeza ajira na uhamishaji wa teknolojia.
Kwa upande wake, ujumbe wa Bunge la Korea uliahidi kuendelea kuhamasisha sekta binafsi na taasisi za Korea kuwekeza nchini Tanzania na kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu unaowanufaisha wananchi wa nchi zote mbili.
Mkutano huo umeonesha dhamira ya pamoja ya Tanzania na Korea Kusini ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara, uwekezaji, maendeleo ya viwanda na uhamishaji wa teknolojia kwa manufaa ya pande zote mbili.
