Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

DK. HASHIL ABDALLAH AKUTANA NA UONGOZI WA TEMDO KUPANGA MKAKATI WA 2025-2030


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara Dkt. Hashil Abdallah amekutana na kufanya mazungumzo na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) pamoja na kujadili mwelekeo wa kimkakati wa Shirika (Strategic Perspective) kuelekea maandalizi ya Mpango Mkakati wa TEMDO (SAP) 2025-2030 , Oktoba 04, 2025 Jijini Arusha.

Katika Kikao hicho Dkt.Abdallah ame amesisitiza kuwa Mikakati wanayoipanga ni lazima uwiane na Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya mwaka 2025 pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.