Habari
DKT.JAFO - RAIS SAMIA MGENI RASMI UZINDUZI KONGANI YA VIWANDA KWALA.
DKT.JAFO - RAIS SAMIA MGENI RASMI UZINDUZI KONGANI YA VIWANDA KWALA.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Kongani ya Viwanda Kwala,Bandari Kavu Kibaha Mkoani Pwani pamoja na Kuzindua Treni ya mizigo (Mgr) utakayofanyika Julai 31, 2025.
Dkt.amesema hayo wakati wa ziara yake ya kuona Maandalizi ya Uzinduzi wa Kongani hiyo Kwala Mkoani Pwani Julai 11,2025.
Dkt.Jafo amesema amefanya ziara hiyo ili kuona maandalizi katika eneo hilo ili kujiridhisha kwa Ufunguzi wa Kongani hiyo ambayo imeshajengwa Viwanda 12 kati ya 250 vinavyotarajiwa Kujengwa.
Aidha Dkt.Jafo amewakaribisha Watanzania wote kujiamda na kushiriki kikamilifu katika uzinduzi huo mkubwa ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Kwa Upande Wake Mkuu Wa Wilaya Ya Kibaha Mkoani Pwani Bw Nickson Saimoni Amesema Eneo Hilo La Ujenzi Wa Viwanda Ni Moja Ya Ongezeko La Uwekezaji Mkubwa Katika Wilaya Ya Kibaha.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon amesema eneo hilo la ujenzi wa Viwanda ni moja ya ongezeko la uwekezaji mkubwa Wilaya ya Kibaha hivyo kukamilika kwa Bandari hiyo ya Kwala pia kutasaidia kupunguza msongamano wa magari ya mizigo bandari ya Dar es Salaam .