Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) kuunga mkono jitihada za matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuwezesha wanawake kutopata madhara kiafya sanjari na vijana kupata ajira hususan wa vijijini kwa kupata umeme wa uhakika
Aidha amesema mabadiliko ya tabia nchi yanagharama kubwa katika nchi hivyo Tanzania imejipanga kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanakuwa kwa kasi katika maeneo ya vijijini na mijini
Rais Samia aliyasema hayo novemba 29, 2024 wakati Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024 na Maadhimishi ya miaka 25 ya Jumuiya hiyo iliyoanza mwaka 1967 na kuvunjika mwaka 1977 kisha kufufuka tena na kufikisha miaka 25 ambapo Wakuu hao wa nchi za EAC walielezea umuhimu wa jumuiya hiyo
Alisema Tanzania inajitajidi kupambana na matumizi ya nishati na ihitaji zaidi ya dola milioni 19 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwaajili ya kurebisha masuala la mazingira hivyo kila wilaya nchini Tanzania ziendeleee kupanda miti ingawa kasi yake ni ndogo.
Alisema wanawake wanapata matatizo mbalimbali kutokana na matumizi ya kuni hivyo lazima kuhakikikisha wanawake wanaondoka na matumizi ya nishati hiyo nawaomba wakuu wa nchi waniunge mkono kuhakikikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
Katika mapambano ya nishati chafu Tanzania inapambana kuhakikisha inasambaza umeme vijijini ili kuwezesha wanawake kupikia na vijana kujiajiri ikiwemo kusambaza umeme wa gesi,kwani nusu ya umeme wa Tanzania unatokana na maji ikiwemo mabwawa ya maji
Alisema katika suala la mabadiliko ya tabia nchi lazima sasa kila Nchi za EAC kukubaliana kwa pamoja ili kuunganisha nguvu na kusisitiza nchi hizo kushirikiana na sekta binafsi ili kuwezesha matumizi ya nishati yanakuwa kwa kasi.
Aidha Alisema Tanzania imekuja na mpango wa BBT kwa kuhakikikisha vijana wanajiajiri katika kilimo,mifugo na Misitu ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo makubwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, utoaji wa ardhi na hati, kujenga makazi na kuwaunganisha katika soko na benki kwa ajili ya mikopo.