Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

kuwezesha vikundi vya maendeleo kunasaidia kujenga uchumi wa wananchi


Waziri wa viwanda na biashara Dkt.Seleman Jafo(Mb) amesema kuwezesha vikundi vya maendeleo kunasaidia kujenga uchumi wa wananchi hasa wanawake kuweza kujipatia fedha na ajira kupitia mradi.

Amebainisha hayo Machi 5,2025 wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Mradi wa Kuongeza thamani za bidhaa taka za plastiki za kutengeneza vigae na Matofali (Zero Waste/Support project for bricks and pavement production) chini ya Women Recycling Foundation Jijini Dar es Salaam.

Dkt.Jafo amesema mradi huo ni Chanzo cha kipato na uchumi kwa wanawake hao pamoja na kuwezesha ufumbuzi wa kutunza mazingira na utengenezaji wa uchumi kwa jamii pamoja na kuondoa changamoto ya uchafuzi wa mazingira.

Aidha amesema ubunifu wao huo ni mustakabli wa maendeleo ya nchi hivyo haina budi kuunga mkono ili kupambana na changamoto za ajira kwa kusaidia serikali na mashirika binafsi kutoa fursa za ajira kwa kupitia miradi kama hiyo.

Dkt.Jafo pia amesema serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara itaendelea kuwaunga mkono ili kusukuma maendeleo mbele kwani utengenezaji wa bidhaa hizo unasaidia kukuza uchumi na kutunza mazingira kwa kuyafanya yawe safi.

Pia Dkt.Jafo ametoa fursa kwa taasisi hiyo kuonyesha bidhaa zao katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba kwa kuagiza Mamlaka ya Maendendeo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kusimamia pamoja na kuielekeza Manispaa ya Temeke kuona namna ya kuwapatia eneo ili kikundi hicho kiwe mfano wa mafanikio kwa wengine.

Kadhalika Dkt.Jafo ameelezea mpango mkakati wa serikali wa ujenzi wa viwanda mbalimbali wa miaka Sita ambapo amewataka wamiliki wa taaisis hivyo kutofumbia macho fursa hiyo.