Habari
erikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanyia biashara kwa kufanya uwekezaji i
Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanyia biashara kwa kufanya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji pamoja na sekta ya Kilimo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) Septemba 10, 2024 wakati akifunga maonesho ya 19 ya Afrika Mashariki yanayofanyika uwanja wa Furahisha tangu Septemba 6 hadi 15, mwaka huu yaliyoandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoa wa Mwanza.
Ameeleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inafanya mazingira yanakuwa wezeshi na watu wanafanya biashara ambapo imeamua kufanya uwekezaji katika Sekta ya kilimo na kwa mwaka 2021 bajeti ya kilimo ilikuwa wastani wa bilioni 294 lakini bajeti ya mwaka 2024/ 2025 ni tirioni 1.2.
"Ni uwekezaji mkubwa na imejielekeza katika kilimo cha umwagiliaji ili kufanya Biashara kufanyika kwa ufanisi, kwani changamoto ya kilimo cha kutegemea mvua imekuwa kubwa hasa wakati mwingine majira hubadilika,"ameeleza Mhe. Jafo.
Pia ameeleza,kuwa serikali imeendelea na juhudi ya kujenga na kuboresha miundombinu kwa kufanya uwekezaji katika ujenzi wa barabara nchi nzima lengo ni wafanyabiashara waweze kufanya Biashara vizuri.
Pamoja na usafiri wa anga,ambapo mpaka sasa Serikali ina ndege 15.Lakini imeendelea kufanya uwekezaji upande wa reli ambapo mpaka sasa kuna treni ya umeme ambayo inatokea Dar-es- Salam hadi Dodoma.
Huku ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ukiendelea kutoka Dodoma,Tabora, Isaka mpaka Mwanza.Pia maungio mengine "connection" yanaenda moja kwa moja mpaka Kigoma, maana yake utakapokamilika utarahisisha ufanyaji wa biashara.
Aidha, uwekezaji mwingine ambao Serikali umefanya ni upande wa Bandari, ambapo uwekezaji mkubwa umefanyika katika Bandari ya Dar-es-Salaam,Mwanza Kasikazini, Kemondo na maeneo mengine lengo ni kurahisha wafanyabiashara kusafirisha na kufanya Biashara.