Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI KURAHISISHA USAJILI WA BIASHARA NA KUKUZA UKUAJI WA BIASHARA NDOGO NA ZA KATI


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo amesema Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya usajili wa biashara, majina ya biashara, alama za biashara, hata za pamoja na huduma za kidijitali ili kurahisisha urasimishaji wa biashara kwa muda mfupi.

Londo ameyasema hayo Aprili 18, 2026 jijini Arusha wakati wa Mkutano wa Biashara ndogo na zakati (SMEs) na Maonesho ya Uwekezaji uliokuwa na kaulimbiu isemayo “Kuharakisha Ukuaji wa SMEs, Utayari wa Uwekezaji na Biashara ya Kimataifa pamoja na Uunganishaji wa Masoko.”

Alisema Tanzania inahitaji kuwa na idadi kubwa ya SMEs zinazozalisha kwa kiwango kikubwa, zinazokidhi viwango na zenye uwezo wa kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi.

Londo ameongeza kuwa licha ya SMEs nyingi nchini kuwa na nguvu na ustahimilivu, bado nyingi zinafanya kazi katika hali ya kujikimu kutokana na changamoto mbalimbali, ikiwemo gharama za kufuata taratibu za kisheria na upatikanaji mdogo wa mitaji.

Kutokana na hali hiyo, amezihimiza SMEs kujikita katika uzalishaji wenye kuongeza thamani, kuhakikisha zinakidhi viwango vinavyotakiwa, kushindana kwa ubora na bei, pamoja na kushiriki katika minyororo ya thamani ya kampuni kubwa, zabuni za Serikali na masoko ya kimataifa.

Aidha, amesitiza matumizi ya teknolojia za kidijitali ili kuongeza wigo wa masoko na kuwafikia wateja wengi zaidi.

Katika hatua nyingine, amezitaja Taasisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA) kuwa muhimu katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinakidhi viwango vinavyotakiwa, akisisitiza pia umuhimu wa kuhamasisha falsafa ya KAIZEN kama utamaduni wa kuboresha uzalishaji endelevu.

Alitaja maeneo yenye fursa kubwa kwa SMEs kuwa ni pamoja na usindikaji wa mazao ya kilimo, sekta ya nguo na ngozi, dawa na vifaa tiba, vifaa vya ujenzi, pamoja na bunifu na sanaa zenye soko la kimataifa.

Pia ametoa wito kwa Taasisi za fedha kushirikiana na SMEs ili kuziwezesha kupata mikopo kwa urahisi na kujiandaa kushiriki kikamilifu katika masoko ya ndani na nje, ikiwemo biashara ya kidijitali.

Kwa upande wa masoko, Londo amesema Sera ya Taifa ya Biashara ya mwaka 2023 inaweka mkazo katika kuimarisha biashara ya ndani, kutumia fursa za masoko ya Kikanda na kimat