Habari
SERIKALI YA TANZANIA NA KENYA ZADHAMIRIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kenya zimejipanga kuendelea kuwasidia Wafanyabiashara kwa kuhakikisha inaondoa vikwazo vya kibiashara baina ya pande zote mbili.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dennis Londo akimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Judith Kapinga katika Kikao cha (10) cha Kamati ya pamoja ya Biashara (JTC) Aprili 17, 2026, Mombasa-Kenya.
Mhe. Londo amesema Wafanyabiashara wa nchi hizo wa nachangamoto zao hivyo kama Serikali ni lazima kuwasaidia ili waweze kufikia malengo yao katika biashara.
Amesema Vikao hivyo ni muhimu kwani vinajadili makubaliano na utekelezaji wake katokana na vikao vilivyopita ili kutekeleza maelekezo ya Marais wa chi hizo pamoja na kuona maeneo gani ya ushirikiano na yapi ya kuboresha ili kurahisisha shughuli za biashara kwa Wananchi wa pande zote mbili pamoja na kunufaika na ujirani mwema na uanachama wa Afrika Mashariki.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwejezaji, Viwanda na Biashara ya Jamhuri ya Kenya Bi. Regina Ombame amesema dhumuni kubwa la kikao hicho ni kuhakikisha hali ya biashara baina ya mataifa hayo mawili inakuwa na ufanisi, usawa na thabiti ili kuwasaidia wafanyabiashara wote.
Kikao hicho cha (10) cha Kamati ya pamoja ya Biashara (JTC) kinalenga kujadili namna ya kuondoa vikwazo vya biashara kilianza Aprili 13-17, 2026 kwa kuqnza na ngazi ya Wataalamu, Makatibu Wakuu na kufikia tamati na ngazi ya Mawaziri.
