Habari
Kamati yaipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Kukutana na Wafanyabiashara.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kufanya Vikao na Wafanyabiashara Nchini.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.David Mwakiposa Kihenzile (Mb) Agosti 17,2023 wakati Kamati ikipokea Taarifa ya Chuo cha Biashara (CBE) pamoja na ya Bodi ya Stakabadhi za ghala katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Mhe.......amesema kuwa Kamati imekuwa ikiona Jitihada za Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu kijaji kuzunguka Mikoa mbalimbali na kufanya vikao na Wafanyabiashara na Wenyeviwanda kwani kwa kufanya hiyo kutasaidia kujua Changamoto zao na kuzifanyia kazi na kuboresha ufanyaji Biashara N…
Kamati yaipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Kukutana na Wafanyabiashara.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kufanya Vikao na Wafanyabiashara Nchini.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.David Mwakiposa Kihenzile (Mb) Agosti 17,2023 wakati Kamati ikipokea Taarifa ya Chuo cha Biashara (CBE) pamoja na ya Bodi ya Stakabadhi za ghala katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Mhe.Kihenzile amesema kuwa Kamati imekuwa ikiona Jitihada za Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu kijaji kuzunguka Mikoa mbalimbali na kufanya vikao na Wafanyabiashara na Wenyeviwanda kwani kwa kufanya hiyo kutasaidia kujua Changamoto zao na kuzifanyia kazi na kuboresha ufanyaji Biashara Nchini.
Aidha Wajumbe walipata nafasi ya kutoa maoni mbalimbali juu ya uboreshaji wa Sekta ya Biashara kupitia Chuo cha Biashara (CBE) pamoja na Bodi ya stakabadhi za ghalani.
Vilevile Kamati imeridhishwa na Mipango ya Chuo cha Biashara(CBE) ya kufikia hatua ya kuanzisha Chuo katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar pamoja na uanzishwaji wa Mfumo utakaowezesha bei za mazao kutoka kwa Wanunuzi wakubwa zinawafikia wakulima.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji wakati akijumuisha maoni na mapendekezo hayo aliishukuru kamati kwa pongezi hizo kwa Wizara pamoja na kuiahidi kamati kuwa ni dhamira yake kuendelea kufanya ziara na kukutana na Wafanyabiashara Nchini kote ili kuhakikisha Wanakuwa na mazingira bora ya ufanyaji biashara