Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Katibu Mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, Prof Adolf Mkenda Ziarani Nchini China.


Katibu Mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof Adolf Mkenda wakutana na wawekezaji kutoka makampuni mbalimbali kwenye Mkutano wa Kuvutia Uwekezaji uliofanyika Ubalozini nchini China. Mkutano huu umehudhuriwa na wawakilishi wa makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza Tanzania. Aidha wamekutana na Uongozi wa Benki ya AIIB iliyoanzishwa kutoa mikopo kwa miradi ya miundombinu kwa nchi wanachama wa Belt&Road. Benki hiyo imeikaribisha Tanzania kujiunga nayo ili iweze kufaidika na fursa za mikopo nafuu. Vilevile, wamekutana na Uongozi wa Kampuni ya Hainan Group (H&A Group) inayomiliki mashirika mbalimbali ya ndege na mahoteli. China imeeleza kwamba katika miaka mitano ijayo itanunua bidhaa kutoka Nje ya nchi zenye thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 24 hivyo nchi za Afrika zina fursa ya kunufaika na soko lake endapo zitajipanga. Kwenye mkutano huo China imeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja za uchumi hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Bagamoyo SEZ. Pia China imeeleza kwamba inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kutekeleza miradi mingine ya ujenzi wa miundombinu.