Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kigahe: Toeni Huduma bora kuilea na kuikuza Sekta Binafsi


Kigahe: Toeni Huduma bora kuilea na kuikuza Sekta Binafsi

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb), ametoa wito wa Mejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya wizara hiyo pamoja na Watumishi kwa ujumla kutoa huduma bora kwa weledi, uadilifu na bidii kwa sekta binafsi ili kuilea na kuikuza ili iweze kuongeza mchango wake katika pato la taifa na maendeleo kwa ujumla.

Kigahe ameyasema hayo Disemba 13, 2024 alipokuwa akifungua Kikao Kazi cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara (NDC, TIRDO, TEMDO, CAMARTEC, SIDO, TBS, BRELA, FCC, FCT, TANTRADE, WRRB CBE, WMA) kilichofanyika Disemba 13, 2024 katika Ofisi za Tume ya Ushindani zilizopo Jijini Dar es Salaam pamoja na kumpokea Naibu Katibu Mkuu Dkt. Suleiman Serera.

Aidha, Kigahe amewasisitiza Wakuu hao kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara inajukumu kubwa katika kuilea sekta binafsi ambayo inatoa ajira kwa watu wengi zaidi, kuchangia katika Pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii kwa Watanzania kwa ujumla.

Akizungumza na Wakuu hao wa Taasisi baada ya kupokelewa na kukaribishwa katika Wizara hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Suleiman Serera ametoa rai kwa Menejimenti ya Wizara na Wakuu hao wa Taasisi kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutekeleza maagizo na maelekezo ya Viongozi mbalimbali wa Nchi na wa Wizara katika kufikia malengo tarajiwa yaliyowekwa katika kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara.

Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara na Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, Prof. Mkumbukwa Mtambo kwa niaba ya Wakuu wa Taasisi hizo amesema Taasisi zote ziko tayari kufuata Maelekezo hayo na kiaidi kutoa ushirikiano katika kila jitihada zinazotekelezwa na Wozara hiyo katika kiendeleza sekta ya viwanda na biashara.