Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kikao cha wadau mbalimbali waliotoa maoni kuhusiana na utafiti wa changamoto za Biashara za mipakani Februari 6, 2025 jijini Dodoma.


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Bw. NeedPeace Wambuya ameongoza kikao cha wadau mbalimbali waliotoa maoni kuhusiana na utafiti wa changamoto za Biashara za mipakani Februari 6, 2025 jijini Dodoma.

Bw.Wambuya amesema Serikali itaendelea kufanya jitihada kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na Biashara wanazozifanya kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugebzi Mtendaji wa Taasisi ya Liberty Sparks, Bw. Evans Exaud amesema kuwa Taasisi imekuwa mstari wa mbele katika kuchochea mijadala na tafiti zinazolenga kuboresha mazingira ya Biashara na Uchumi nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikitilia mkazo ujumusihaji wa jinsia katika Biashara,upatikanaji wa taarifa za masoko,biashara huria na mabadiliko ya sera yanayolenga kukuza ushindani na ufanisi katika sekta ya viwanda, kilimo na madini.

“Ripoti inayojadiliwa na kuzinduliwa leo inatokana na mchango mkubwa wa wadau kutoka sekta mbalimbali ambayo inatoa hali ya biashara za mipakani, changamoto zilizopo na mapendekezo ya maboresho ya mazingira hayo katika sekta za viwanda, kilimo na madini,”alisema

Aliongeza kuwa :”Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya viwanda, kilimo na madini zinakuwa sehemu ya ukuaji wa biashara mipakani kupitia sera na mikakati mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya mipakani, kuimarisha ushirikiano wa kikanda,kuwezesha wafanyabiashara wadogo na kati na kupunguza vikwazo vya biashara,”

Liberty Sparks ni taasisi ya elimu na utafiti inayojikita katika kukuza uwezeshaji kiuchumi kupitia biashara huru na mabadiliko ya kibiashara.

‘'Taasisi inaamini kuwa kupitia sera sahihi, utafiti wa kina na wadau utasaidia kufanikisha maendeleo ya biashara mipakani na sekta nyingine muhimu za kiuchumi,”amesema Exaud.