Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe ameongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Misri na Tanzania kutembelea Kongani ya Viwanda vya kuchakata mazao la SILO FOODS for Food Industries katika Mji wa Sadat nchini Misri Januari 26, 2025
Viwanda hivyo vinajishughulisha na uchakataji wa mazao kama ufuta, ngano na maziwa na kisha kuzalisha bidhaa mbalimbali za vyakula kama vile Unga wa ngano, Snacks, Biskuti, Tambi, Pasta, Chocolate, Mikate, Maziwa, Yoghurt, n.k.
Aidha, kabla ya kutembelea viwanda hivyo, ujumbe huo ulitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi wa ILMONTE katika eneo la Galala, Sokhna Misri.
Lengo la ziara hizo ni kujufunza, kubadiloshana uzoefu pamoja na kuwahamasisha wawekezaji kutoka Misri kuja kuwekeza Tanzania.
Katika Ziara hiyo, Mhe. Kigahe aliambatana na Mhe. Balozi Richard Makanzo ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dkt. Stephen Nindi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo pamoja na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania.
Kongamano la Biashara na Uwekeza kati ya Misri na Tanzania linafanyika nchini Misri kuanzia tarehe 23/1/25 hadi tarehe 1/2/25 katika miji ya Cairo, Alexandria na Aswan.