Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

LONDO INSPECTS LABORATORIES AT TBS


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo (Mb) akitembelea Maabara mbalimbali zilizopo katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa ziara yake ya kutembelea Shirika hilo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika pamoja na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo Julai 27,2026 Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Londo ametembelea Maabara hizo ikiwemo maabara za chakula, vifaa vya umeme, uzito na vipimo mbalimbali ili kuona uteukelezaji wa majukumu ya shirika hilo katika kusimamia viwango vya bidhaa na kulinda maslahi ya walaji.