Habari
Matumizi ya Alama ya Biashara na Huduma ya Tanzania (MADE IN TANZANIA) itasaidia bidhaa kutambulika kimataifa.
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa matumizi ya Alama ya Biashara na Huduma ya Tanzania (MADE IN TANZANIA) itasaidia bidhaa kutambulika kimataifa.
Amebainisha hayo katika Ufunguzi wa Kongamano la Made in Tanzania iliyofanyika katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) Julai 08,2025.
Mhe.Kigahe amesema kuwa kuwepo kwa Nembo hiyo kutasaidia utambulisho wa bidhaa inapotoka kwasababu bidhaa nyingi zinazozalishwa Tanzania zinakuwa hazitambuliki kwa urahisi katika Masoko ya kimataifa ikiwemo Kahawa na Asali.
Aidha Mhe.Kigahe ametoa rai kwa Wafanyabiashara nchini kutumia nembo hiyo ili bidhaa zao ziweze kutambulika kirahisu zaidi katika masoko hayo ili kupata soko zaidi.