Habari
Mafanikio ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara Katika Kipindi cha Siku 100

MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA KIPINDI CHA SIKU 100 WAKATI WA MAHOJIANO YA MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE, (MB.), WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI NA TELEVISHENI YA TBC TAREHE 10 FEB. 2016 MWELEKEO WA SERIKALI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo mkubwa katika ujenzi wa Viwanda, na katika Hotuba ya Rais aliyoitoa Bungeni alisisitiza kuwa sekta ya viwanda ina jukumu kubwa la kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025. Dhana ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano ni kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kichumi na maendeleo ya jamii. DIRA YA WIZARA (VISION) Kuwa msingi wa ushindani wa viwanda unaowezesha kukua kwa uchumi endelevu na shirikishi DHIMA YA WIZARA (MISSION) Kujenga msingi shindani na endelevu wa viwanda wenye kuwezesha biashara ulimwenguni kwa kuzingatia faida za mahala tulipo kijiografia na rasilimali zilizopo nchini kupitia Sera, Mikakati na Mipango kwa mageuzi shirikishi ya viwanda. MAJUKUMU YA WIZARA (i) Kuandaa, kuratibu na kupitia Sera na Mikakati ya Sekta za Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji; (ii) Kufuatilia na kuperemba (Monitoring and Evaluation-M & E) utendaji katika sekta za Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji; (iii) Kubuni na kuandaa programu za kuendeleza sekta za Wizara; (iv) Kukusanya, kuchambua, kutathimini na kusambaza taarifa za sekta za Wizara; (v) Kukuza na kuhamasisha biashara ya ndani na nje; (vi) Kuimarisha utafiti wa maendeleo ya viwanda; (vii) Kuimarisha ufanisi wa utendaji wa wafanyakazi wa Wizara na Taasisi zake; (viii) Kuboresha upatikanaji wa huduma za kuendeleza biashara; (ix) Kusimamia utekelezaji wa sheria zinazosimamia Sekta tajwa; (x) Kuboresha mazingira ya utendaji kazi ya Sekta Binafsi; na (xi) Kutafuta fursa za masoko ya bidhaa na huduma za Tanzania. 1) SEKTA YA VIWANDA MIKAKATI NA UTEKELEZAJI KATIKA KUENDELEZA SEKTA YA VIWANDA, Katika siku mia moja za Serikali ya awamu ya tano Wizara imefanikiwa 1. Eneo la TAMCO – KIBAHA Wizara kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) imefanikiwa kupata wawekezaji wa aina tatu kwa ajili ya kuwekeza kwenye i. Kufungua kiwanda cha kutengeneza madawati kwa ajili ya shule za Sekondari. Kampuni inajulikana kwa jina la EDOSOMA HARDWARE LTD; ii. Kiwanda cha kuunganisha magari (Motor Vehicle Assembling Plant). Kampuni inajulikana kama TATA AFRICA HOLDING LTD; na iii. Kiwanda cha kutengeneza Madawa ya Binadamu hususan Intravenous (IV) Fluids (Pharmaceutical Plant). Mradi huu utatekelezwa na NDC kwa kushirikiana na mwekezaji, Kampuni ya Pharmaceutical Limited ya China. Uwekezaji unatazamiwa kuwa wa dola za Kimarekani milioni 197. Kwa kuanzia kiwanda kitaajiri wafanyakazi 100. 2. Kuendeleza viwanda vilivyobinafsishwa. Katika kutekeleza sera ya mageuzi ya uchumi iliyokwenda sambamba na ubinafsishaji wa mashirika ya umma, jumla ya viwanda 113 vilibinafsishwa. Kati ya hivyo, viwanda 79 vinafanyakazi kwa sasa na 34 vimefungwa (Zaidi ya nusu wameshawasilisha taarifa zao kwa TR) Katika kutimiza azma ya Rais ya kutwaa na kurudisha Serikalini viwanda vya umma vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi kutokana na wawekezaji kushindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba; Wizara yangu kupitia Msajili wa Hazina imefanikiwa kutwaa Kiwanda cha Chai cha Mponde kilichopo katika jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga. Kiwanda hicho kilitwaliwa kutokana na mwekezaji, Umoja wa Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA) kushindwa kutekeleza Mkataba wa Mauzo. Tunaendelea kupitia mikataba ya mauzo ya viwanda vingine vyote. 3. Mamalaka ya Maeneo Huru ya Uzalisha kwa Mauzo Nje (EPZA) imesajili Kampuni ya ALISTAIR FREE PORT LTD kuwekekeza katika eneo la Mtwara Free Port Zone. Kampuni inatazamia kuwekeza Dola za Kimarekani 700,000 kwa ajili ya eneo la Kutunzia Mizigo (Cargo Storage). 4. Niliagiza kufanya tathmini ya viwanda vyote vya nguo na mavazi nchini. Taarifa inaonyesha kwa sasa kuna:- (i) Viwanda 16 vinafanya kazi. Kati ya hivyo, 15 ni vikubwa na kimoja ni kidogo. Viwanda hivyo vimeajiri jumla ya wafanyakazi 17,600; (ii) Viwanda 8 vimefungwa. kati ya hivyo, 6 vilikuwa vya umma vikabinafsishwa kwa sekta binafsi. 5. Kiwanda cha Viuadudu cha Kibaha: Tumeainisha matatizo ya kiwanda hiki na kukubaliana na Balozi wa Cuba nchini kuwa uzalishaji wa kibiashara uwe umeanza katika kipindi cha miezi mitatu. 6. Maeneo ya Viwanda: Tumewaandikia Halmashauri za Wilaya zitenge maeneo ya viwanda na biashara. Tayari Halmashauri ya Mkuranga, Pwani imeshatenga eneo kubwa la ekari 700 ambapo kwa kuanzia wataanza kuendeleza ekari 360. Tunashirikiana na Halmashauri hiyo kupata wawekezaji katika eneo hilo. 7. Tulikutana na Balozi wa India nchini mwezi wa Januari na kujadili juu ya ushirikiano katika biashara ya uwekezaji tulikubaliana pia kuwa Mradi wa Supporting Indian Trade and Investment for Africa (SITA) ambao kwa Tanzania unalenga kuongeza thamani mnyororo wa mazao ya Pamba, Ngozi, Mafuta ya Alizeti na Mazao Jamii ya Kunde (Pulses) uendelee kutekelezwa. Tayari Mikakati kwa sekta za Pamba, Ngozi na Mafuta ya Alizeti na Mpango Kazi kwa mazao Jamii ya Kunde (Pulses) zimeandaliwa. 8. Tumeagiza Mamlaka ya EPZ kukamilisha suala la eneo la Kurasini Logistic Centre haraka ili uwekezaji uanze mara moja. Tumeomba Serikalini kiasi cha Tshs. Bilioni 3.7 kilichobaki ili kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi 15 waliobaki na kiasi kingine kutumika kwenye ubomoaji na usafi wa eneo kwa ujumla. Kukamilika kwa mradi huu kutatoa ajira zipatazo 25,000. Uwekezaji katika eneo hilo utasaidia upatikanaji wa fedha haraka zitakazosaidia uwekezaji katika maeneo mengine. 9. Tumeangalia matatizo yanayokwamisha kuanza kwa miradi mikubwa na ya kimkakati ya: (i) Mchuchuma na Liganga. Miradi hii inatarajiwa kuajiri wafanyakazi wa moja kwa moja 6,000 na wasio wa moja kwa moja (indirect) 24,000; (ii) Mradi wa Magadi (Soda Ash) wa Engaruka ambao nao utaajiri takriban wafanyakazi 500 wa moja kwa moja na 2,000 wasio wa moja kwa moja. 10. Kiwanda cha General Tyre tayari Serikali ilikwishanunua hisa 26% zilizokuwa zinamilikiwa na mbia mwenza (Kampuni ya Continental AG). Shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kufufua Kiwanda hicho zitapatikana kutoka mabenki ya ndani. Umiliki wa hisa asilimia 100 za General Tyre unahamishiwa chini ya NDC na Tamko la Serikali (Government Notice-GN) ya kuhamisha itatoka wakati wowote. 2) SEKTA YA VIWANDA VIDOGO NA BIASHARA NDOGO 1. Tumekubaliana na Balozi wa India nchini Tanzania kuwa nchi ya India kupitia National Small Industries Corporation (NSIC) na tumekubaliana kuwa NSIC itasaidia SIDO kujenga Incubators 20 za mfano. 2. Wizara kupitia SIDO, imefanikiwa kutengeneza mashine moja ya kukamua mafuta ya alizeti (Refinery) ambayo kwa sasa inafungwa huko Mkoani Geita. 3. SIDO kushirikiana na Serikali ya Canada wameafikiana kuanzisha Programu ya Kujenga uwezo wa wajasiriamali wa kati kuweza kufikia masoko ikiwa pamoja na kuhudumia makampuni makubwa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Iringa na Mwanza. 4. Idara imetembelea manispaa ya Ilala kuona maeneo yaliyotengwa na kuendelezwa kwa ajili ya shughuli za wajasiriamali. 5. Pamoja na hilo wizara imehamasisha Halmashauri za Miji na Wilaya kutenga maeneo ya uwekezaji kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati. 3) SEKTA YA BIASHARA 1) Tulikutana na Balozi wa India nchini mwezi wa Januari na kujadili juu ya ushirikiano katika biashara ya uwekezaji ambapo alieleza nchi ya India imeongeza bidhaa zinazoingia kwenye Duty Free Tariff Preference (DFTP) inayotoa upendeleo (preference) kwa mazao (commodities) yanayouzwa nchini India kutoka nchi Maskini Duniani (LDCs) hadi zaidi ya bidhaa 468. 2) Katika kukuza na kuendeleza sekta ya biashara katika mkutano wa kumi uliofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 15 hadi 19 Desemba, 2015. WTO (10th MINISTERIAL Conference) Serikali kupitia Wizara yangu imefanikiwa:- Kufikia makubaliano ya kulegeza na kurahisisha vigezo vya uasili wa bidhaa katika masoko ya upendeleo ambapo nchi itaweza kutumia kikamilifu masoko ya upendeleo kwa bidhaa za Tanzania kuingia kwa urahisi katika masoko hayo. Makubaliano yanazitaka nchi tajiri zitekeleze ifikapo mwaka 2016 na nchi zinazoendelea mwaka 2018; 3) Takwimu za Jarida Maridadi la The Economist la Pocket World in Figures 2015 zinaonyesha Tanzania kuwa ni nchi ya 17 duniani katika kasi ya ukuaji wa viwanda. 4) Kwa mujibu wa World Investment Report 2015, Tanzania imekuwa chaguo Na. 1 kwa wawekezaji katika Kanda ya EAC (Tanzania is the preffered destinations for industrial investment in the region). Hali hii ni matokeo ya uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji. Hali hii imefanya agizo litolewe kwa Viongozi wa Mikoa na Halmashauri kutenga maeneo mahsusi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda. 5) Tanzania imeweza kufanya vizuri kwenye urari wa biashara katika siku 100 (Novemba - Januari) zilizopita kwenye baadhi ya masoko muhimu kama inavyoonekana katika Jedwali hapo chini. NAMBA NCHI MAUZO YA NJE UIGIZAJI WA BIDHAA KUTOKA NJE URARI WA BIASHARA (MAUZO-UAGIZAJI) 1 India 631,866,747,912 478,821,725,970 153,045,021,943 2 Kenya 241,122,744,372 125,354,181,471 115,768,562,901 3 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 211,375,028,093 40,023,105 211,335,004,988 4 Ufaransa 293,301,316,333 46,657,500,449 246,643,815,883 5 Comoro 406,158,634,745 29,789,130 406,128,845,616 6 Uswisi 100,613,490,476 59,491,714,712 41,121,775,764 JUMLA 1,884,437,961,931 710,394,934,836 1,174,043,027,095 a) Wizara imeshiriki katika Mkutano wa 27 wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara (Committee of Ministers of Trade) wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika mnamo tarehe 20 Novemba, 2015 mjini Gaborone, Botswana. Pamoja na mambo mengine, Mkutano huu ulipitia maombi yaliyowasilishwa na Tanzania kuhusu bidhaa za Sukari na Karatasi kulipiwa ushuru pindi zinapoingia Tanzania kutoka nchi wanachama wa SADC kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia 2015/2016 hadi 2017/2018. b) Wizara ilishiriki katika Mkutano wa 19 wa Kikanda unaohusu Uondoaji wa Vikwazo vya Kibiashara Visivyokua vya Kiushuru (NTBs) uliofanyika mjini Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 8 hadi 10 Desemba, 2015. Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo ulipitia taarifa za Kamati za Kitaifa zinazo shughulikia Vikwazo Vya Biashara Visivyokuwa vya Kiushuru (NTBs) na kupitia Bango Kitita (Time bound Matrix) la uondoaji wa Vikwazo Vya Biashara Visivyo kuwa vya Kiushuru (NTBs). Katika kikao hicho taarifa ilitolewa kuwa kulikuwa na Vikwazo mbalimbali vya kibiashara vipatavyo 128 ambapo kutokana na juhudi za Kamati ilifanikiwa kuondoa vikwazo104 na kubakiwa na vikwazo 23. ==== Wito Kwa Wafanyabiashara Wa Kitanzania Kuwa Vikwazo Hivi Vipo Pia Katika Nchi Wanazofanya Nazo Biashara. Tafadhali Watoe Taarifa Kwa Serikalii Na Hata Vyama Vyao Vya Biashara Ili Tukikutana Katika Vikao Hivi Tuweze Kuvijadili c) Wizara ilishiriki katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta ya Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha, Tanzania mnamo tarehe 9 hadi 13 Novemba, 2015. Pamoja na mambo mengine Mkutano huu uliridhia kutengeneza vigezo ambavyo vitakitambua chuo cha Usimamizi wa Kodi-Institute of Tax administration (Tanzania) kuwa Centre of Excellence kwenye mafunzo yote yanayohusu Forodha na Kodi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia ilikubaliwa kuandaa miongozo ya Mawakala wa Forodha wa Jumuiya ya EAC nakuandaa Mkakati wa Kiforodha wa Kikanda (EAC) kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2016-2021. 4) SEKTA YA MASOKO • Kwa kipindi cha kuanzia mwezi Novemba, 2015 hadi Januari, 2016, Wizara imetoa jumla ya leseni 1,782 ikilinganishwa na Leseni 1,106 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2014 hadi Januari, 2015. Ongezeko hilo ni sawa na aasilimia 61. Aidha, maduhuli ya Serikali yaliongezeka na kufikia Shilingi 1,572,110,159 kutoka Shilingi 879,558,531 katika vipindi hivyo. • Wizara imeendelea kuhakikisha kuwa Halmashauri zote za Majiji, Manispaa, Miji na Miji Midogo pamoja na Halmashauri za Wilaya zinapata vitabu vya leseni za biashara kwa wakati. Katika kipindi cha robo ya pili cha Oktoba – Desemba 2015, jumla ya vitabu 290 vya leseni za biashara vilitolewa na kusambazwa nchini kote ikilinganishwa na vitabu 600 vilivyo sambazwa katika robo ya kwanza. • Katika kuendeleza, kukuza na kulinda maslahi ya waandishi, wasanii wafasiri, watayarishaji wa kurekodi sauti, watangazaji, na wachapishaji, Wizara kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA imefanikiwa kufanya usajili wa Wanachama wa muziki 42, kusajili kazi za muziki 468 na kutoa hati za uthibisho wa kazi za muziki 94; Pia kutoa usajili wa wanachama wa Filamu 16, na kusajili kazi za filamu 68 na hati za uthibisho wa kazi za filamu 104; aidha, Wizara imefanikiwa pia kufanya usajili wa Wanachama wa kazi za maandishi 103, kazi za maandishi 131 na hati za uthibisho wa kazi za maandishi 59. UWEKEZAJI NA UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA BIASHARA Tumeendelea Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Biashara ambapo: i. WAKALA WA USAJILI WA MAKAMPUNI NA LESENI (BRELA) 4.1 Mafanikio ya huduma kwa njia ya mtandao. Mafanikio ya kutoa huduma kwa njia ya mtandao hususan Kusajili Majina ya Biashara, Kutoa taarifa za makampuni na Majina ya Biashara na uhakiki (due diligence), kupitisha majina ya usajili na kufanya malipo kwa mtandao ni kama yafuatayo:- • siku za usajili wa Majina ya Biashara zimepungua kutoka siku moja hadi masaa mawili ikiwa Mteja amekamilisha taratibu zote. • Gharama za mteja kupata huduma zimepungua mara dufu kwa kuwa Mteja halizimiki kufuata huduma Dar es salaam kama ilivyokuwa kabla ya kutoa huduma kwa njia ya mtandao • Kuongeza ufanisi wa utoaji huduma BRELA • Maombi ya usajili yameongezeka. • Malalamiko ya ucheleweshaji huduma yamepungua kwa kiasi kikubwa. Taarifa ya Utekelezaji wa Usajili kuanzia tarehe 1.11.2015:- a) Maombi ya Makampuni (Company Registration) Siku 100 yaliyopokelewa 2,375 na kati ya hayo 2,295 yalisajiliwa (Makampuni 80 yalikuwa yanasubiri kukamilisha matakwa mbali mbali ya kisheria) – siku 3 tu kusajili Julai – Novemba yalisajiliwa 2,101 tu, hivyo kasi ya utendaji imeongezeka b) Maombi ya usajili wa Majina ya Biashara (Business Names) yalipokelewa 2,420 kati ya hayo majina 2,416 yalisajiliwa kwa njia ya mtandao ikiwa ni zaidi kwa asilimia 20 ya majina yaliyosajiliwa kwa kipindi cha siku 100 zilizopita ambapo yalisajiliwa majina 2,017. Ndani ya siku moja, hata masaa 2 au 3, maximum siku 1. c) Alama za Biashara na Huduma (Trade Marks) zilizopokelewa na kushughulikiwa ni 833 ambapo kwa kipindi cha nyuma kama hicho tulipokea na kushughulikia Alama 786 ambapo ni ongezeko la asimilia 6. d) Hataza (Patents) zilizopokelewa na kufanyiwa kazi ni 7 na kwa kipindi kama hicho cha nyuma zilipokelwa Hataza 7. e) Maombi ya Leseni za Viwanda (Industrial Licences) zilizopokelewa ni 23 na leseni zilizotolewa ni 22. Kwa kipindi cha nyuma kama hicho zilizotolewa leseni za viwanda 20 ikiwa ni ongezeko la asimilia 10. f) Wakala ilipokea jumla ya maombi ya taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara (official Searches) 2315 yaliyoombwa na Taasisi mbali mbali na watu binafsi kwa ajili ya kuhakiki (Due diligence) kwa njia ya Mtandao na yaliyojibiwa ni 2,305. Kwa kipindi cha nyuma kwa muda kama huo maombi yaliyojibiwa ni 719. Kabla ya hapo Mwombaji alihitajika kuandika barua BRELA au kufika binafsi. Kwa sasa maombi ya taarifa yanafanyika na kujibiwa kwa njia ya Mtandao. Utaratibu huu umeleta ufanisi kwa kurahisisha kupata taarifa za uhakika na pia kupunguza gharama kubwa kwa wananchi na taasisi mbali mbali za binafsi na za Serikali. Barua hizo za maombi ya taarifa na uhakiki zinajibiwa ndani ya siku mbili za kazi tangu zilipopokelewa. g) Pia Wakala hupokea na kuidhinisha maombi ya Majina ya Makampuni na majina ya Biashara yanayokusudiwa kusajiliwa. Maombi 6,559 ya Majina ya Makampuni na Majina ya Biashara yalipokelewa na kupitishwa. Ambapo kwa kipindi cha nyuma kwa muda kama huo ni 6,425. Mfumo huu umeondoa utaratibu wa awali wa kuandika barua za maombi ya kuidhinisha majina kabla ya Mteja kuandaa Katiba ya Kampuni (Memorandum and Article of Association) kwa sasa huduma hii inapatikana kwenye mtandao na kupunguza muda wa kupitisha majina. 4.2 Agizo la Serikali la kusimamia na kujaza fomu za hati ya uadilifu na maadili kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi limetekelezwa na makampuni 1120 yamekwisha kujaza fomu hizo. 4.3 Mtaalam wa kutengeneza mfumo wa kusajili kwa njia ya mtandao (Online Registration systems) ambayo itajumuisha mifumo yote ya shughuli za BRELA ikiwepo usajili wa Makampuni, Usajili wa Majina ya Biashara, Alama za Biashara na huduma, Kutoa Hataza na Leseni za Viwanda amepatikana. Aidha Mfumo huu utawezesha kuunganishwa na masijala na taasisi zinazofanya shughuli zinazotegemeana kama vile TIC, TRA, NIDA, RITA n.k ili kuleta ufanisi na tija kwa wateja na wawekezaji. Mradi huu unategemewa kuwezesha kuwepo na “ an elecronic one stop shop’. Kazi hii inategemewa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi saba kuanzia mwezi Machi 2016. 4.4 Wakala imeanzisha dawati maalum la elimu kwa wateja hususan kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kwa ajili ya kusajili Majina ya Biashara, Kutoa taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara na uhakiki (due diligence), kupitisha majina ya usajili na malipo kwa mtandao katika ‘ground floor’ katika jengo jipya la ushirika, Mnazi mmoja. Pia mafunzo yanatolewa kwa maafisa Biashara na maafisa wa TCCIA kanda ya Kaskazini na wa Mkoa wa Kigoma ili wateja waweze kupata huduma popote na kwa msaada katika ngazi ya wilaya. Aidha, Wakala imetenga fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa mikoa iliyobakia. 4.5 Tovuti ya wakala www.brela.go.tz imeboreshwa ili kuweza kwenda sambamba na tekinologia ya sasa, kuweza kutoa huduma ya usajili kwa njia ya mtandao na kuwa rafiki kwa watumiaji. Aidha tovuti imeboreshwa na kuwa elimishi kwa wadau wote. Taratibu za usajili pamoja na ada zote zimewekwa kwenye tovuti. (i) TBS • Imeajiri wafanyakazi zaidi (200) ili kuweza kutoa huduma vizuri na kwa haraka katika maeneo yote yakiwepo ya mipakani. • TBS limeanza kufanya kazi bandarini kwa masaa 24 ili kuhakikisha wafanyabiashara wasio waaminifu hawaondoi bidhaa zao katika bandari hiyo na kuingiza soko la ndani bila kuzithibitishwa. • TBS limefanikiwa kuongeza idadi ya wafanyakazi katika vituo vya mipakani. (ii) FCC - Imeendelea kufanya ukaguzi wa bidhaa kwenye maduka na sokoni kubaini bidhaa bandia (FEKI). • Hivi karibuni (4 Feb 2016) FCC ilikagua na kukamata Kalamu FEKI aina ya OBAMA katika maeneo ya Kariakoo. Jumla ya kalamu 353,700 zenye thamani ya Tsh. 7. 74 mil zilikamatwa. Zoezi la kukagua bidhaa feki ni mwendelezo. • Wizara kupitia Baraza la Ushindani kuanzia mwezi Novemba 2015, imeweza kusikiliza na kutolea maamuzi kesi za rufaa 2 kati ya 4 na Kesi za Maombi ya Gharama (Bill of Cost) 3 kati ya 7 zitokanazo na Mamlaka za Udhibiti na Ushindani ndani ya soko (EWURA, TCRA, TCAA, SUMATRA pamoja na Tume ya Ushindani (FCC). (iii) TIRDO - Wizara kupitia Shirika la TIRDO, imeweza kuboresha maabara ya nishati kwa kununua vifaa vinavyoweza kupima sampuli za makaa ya mawe na kuweza kujua ubora wake. Vifaa hivi vitasaidia Wizara kuishauri serikali kuhusu ubora wa makaa ya mawe yanayopatikana nchini na hivyo kuongeza pato la Taifa litakalotokana na usafirishaji na matumizi ya makaa hayo. Maabara inakwenda sambamba na kufanya utafiti wa nishati mbadala na kubuni tekinolojia za matumizi bora ya makaa ya mawe viwandani na majumbani. (iv) WMA – Tumeimarisha usimamizi wa vipimo katika shughuli za bandari hasa kwenye upakuaji wa mafuta. Tutaendelea kushirkiana na Taasisi zingine kuhakikisha Serikali haipotezi mapato yake. (v) CAMARTEC - Toka awamu tano kuanza, kwa kipindi cha miezi mitatu (3) Kituo (CAMARTEC) kimetengeneza mashine 15 za kufyatulia matofali ya gharama nafuu (Cinvaram machine) zilizoagizwa na AWF kwa ajili ya kuwasaidia wa wananchi waishio maeneo ya Ngorongoro. Mashine hizi ni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na zina uwezo wa kufyatua matofali 200 kwa siku kila moja. Vilevile CAMARTEC iliweza kutoa mafunzo kwa wananchi 30 kwa ajili ya matumizi ya mashine hizo. • Vile vile, Kituo kimejenga mitambo 4 mikubwa ya biogesi yenye ukubwa wa 60m3 katika Gereza la Karanga na Shule ya Sekondari Visitation Mkoani Kilimanjaro. Mitambo hii inayotumia kinyesi cha ng'ombe na Binadamu itasaidia kutunza mazingira kwa kupunguza maatumizi ya kuni na kuifadhi mazingira. • Kupitia Mradi wake wa TDBP (Tanzania Domestic Biogas Programme) unaojenga mitambo midogo ya katika ngazi ya kaya, kituo kimejenga mitambo 527 kwenye maeneo ya ukanda wa ziwa, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Njombe na Mbeya ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa watumiaji. TDBP imetoa mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamili ambao wameunda kampuni zao za ujenzi wa mitambo na hivyo kutengeza zaidi ya ajira 400. (vi) Tumeziagiza taasisi zetu za TIC, TBS, FCC, TRA, Uhamiaji kufanya kazi kwa karibu sana ili kutoa huduma stahiki kwa haraka na kuondoa kero kwa wawekezaji na wafanyabiashara; BODI YA STAKABADHI GHALANI Maboresho ya Sheria inayosimamia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala • Bodi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imeandaa kanuni za Mfumo ili kukidhi maboresho yaliyofanyika katika Sheria ya Mfumo. Maboresho hayo yanalenga kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mfumo na pia kukidhi mahitaji ya soko la bidhaa(Commodity Exchange Market) lililoanzishwa. Mfano wa changamoto zilizokuwepo ni utambuzi wa wadau wakuu wa mfumo. Awali aliyekuwa anatambulika ni Mwendesha ghala tu ambapo kwa sasa wadau wakuu wengine wamejumuishwa ambao ni wakulima, taasisi za fedha, Wanunuzi wa bidhaa, Meneja dhamana. Kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala • Jumla ya Mazao yenye uzito wa tani 140,838 za Korosho, Kahawa na Mahindi zimekusanywa kupitia mfumo wa Stakabadhi za ghala. Kiasi cha kilo 127,831 yenye thamani shilingi 320 billioni ambapo fedha hizi ni mapato kwa wakulima, watoa huduma na halmashauri kiasi • Malipo kwa wakulima ni kama ifuatavyo hadi sasa:- 1. Chama Kikuu cha Mtwara Masasi (MAMCU Ltd) kimewalipa wakulima malipo ya kwanza na ya pili jumla ya shilingi billion 52.6 na bonasi ya shilingi bilioni 35.4. 2. Chama Kikuu cha Ruangwa Nachingwea Liwale (RUNALI) kimewalipa wakulima malipo ya kwanza na ya pili jumla ya shilingi billion 23.4 na bonasi ya shilingi bilioni 16.7 3. Chama Kikuu cha TANECU kimewalipa wakulima malipo ya kwanza na ya pili jumla ya shilingi billion 71.0 na bonasi ambayo haijalipwa haitakuwa chini ya shilingi bilioni 48.0 • Ushuru wa zao unakusanywa na halmashauri husika kiasi cha shilingi billioni 2.6 zimekusanywa katika wilaya za Mtwara, Masasi na Nanyumbu (MAMCU Ltd) na shilingi billioni 1.2 katika wilaya za RUangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI) na shilingi 3.6 bilioni katika Wilaya za Newala na Tandahimba (TANECU). Mikopo Kwa Wakulima • Kiasi cha shilingi Bilioni 25 zimetolewa kwenye zao la kahawa korosho shilingi billion 65 na mahindi millioni 100 kama mkopo kupitia mfumo wa Stakabadhi za ghala Tanzania. Tadhimini ya utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala • Kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Kilimo na Chakula serikali imefanya kutadhimini ya utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwenye maeneo mbali mbali ambako mfumo unatekelezwa hususani katika zao la Korosho. Mapendekezo ya wataalam yatazingatiwa katika KITUO CHA UWEKEZAJI (TIC) • Jumla ya maombi 34 ya miradi ya uwekezaji yalipokelewa na Kituo cha Uwekezaji kwa lengo la kusajiliwa ambapo kati ya maombi hayo 30 yalikidhi sifa na kupitishwa. Miradi iliyosajiliwa inatarajia kuwekeza jumla ya dola za Kimarekani milioni 453.85 na kutoa ajira kwa watanzania zipatazo 8,233 • Miradi iliyosajiliwa ilikuwa kwenye sekta tatu (3); sekta ya viwanda na usindikaji miradi 18, kilimo miradi 2 na vilevile utalii miradi 2. • Kati ya miradi 30 iliyosajiliwa kwa kipindi hiki, 15 inamilikiwa na Watanzania, 11 wageni na 4 ubia • Muda wa kupitia miradi ya uwekezaji mpaka hatua ya kuisajili ya umepungua kutoka siku 14 mpaka siku 10 • Muda wa kuidhinisha vibali vya uhamiaji na kazi umepungua kutoka siku 30 mpaka siku 15 kutokana na ufanisi wa maofisa wa kazi na uhamiaji waliopo TIC • Katika kipindi hicho jumla ya makampuni 12 yalisajiliwa na afisa kutoka BRELA na leseni za biashara 19 zilitolewa kupitia Afisa Biashara wa Wizara aliyepo TIC • Huduma za ardhi zinazotolewa Kituoni zimefanyika vema. Mfano Kitengo kimefanikiwa kushughulikia jumla ya maswala mbali mbali ya ardhi yapatayo 255 ikiwemo kufuatilia hati za wawekezaji wizarani, kuhudhuria vikao vya kujadili masuala ya ardhi, kutoa ushauri wa masuala ya ardhi kwa wawekezaji na kuhudhuria vikao maalumu vya masuala ya ardhi. Aidha jumla ya hati 5 zisizo za asili ‘’Derivative title’’ zilipokelewa na kushughulikiwa na 1 ipo katika hatua za mwisho kukamilika • Huduma za TRA kwa wawekezaji zimeendelea kutolewa ambapo wateja 489 walihudumiwa kwa mchanganuo ufuatao. Kitengo kimeweza kutoa elimu kwa walipa kodi wapatao 405, kutembelea miradi 9 kwa ajili ya uhakiki, kufanya mikutano 6 na kutoa misamaha ya kodi 69 tu. .