Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Thomas Terstegen


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Thomas Terstegen na Ujumbe wake katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2024.

Ugeni wa balozi huyo akiwa ameambatana na ujumbe wake na Wawekezaji wa Viwanda vya Magari ikiwemo Kampuni ya kutengeneza Magari ya Volkswagen umelenga katika kuunda Magari na kushirikiana na wadau wengine katika kutengeneza vifaa vya magari pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kuimarisha Sera ya Viwanda vya magari Nchini.