Habari
Mhe Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb) amefungua rasmi kongamano la biashara baina ya Tanzania na nchi ya Iran
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb) amefungua rasmi kongamano la biashara baina ya Tanzania na nchi ya Iran, ambapo ni siku ya kwanza ya kongamano hilo litakalofanyika kwa siku nne kuanzia leo tarehe 16 hadi 19 Oktoba 2024 likihusisha Viongozi, wafanyabiashara na wadau wa sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja Kilimo, Ufugaji, Ujenzi, Madini na nyinginezo wakijadili namna ya kushirikiana katika kubadilishana na kutumia fursa zilizopo pande zote mbili na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa nchi hizi.
Kongamano hilo la Biashara baina ya Tanzania na Iran limeratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na linafanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere maarufu kama (Sabasaba), Kilwa Road Dar es Salaam.