Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir akipokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo(Mb) -alipo wasili nchini leo tarehe 30 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024.
Mapokezi hayo halifanyika alipo wasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi
umetanguliwa na Kikao cha Ngazi ya Juu kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye kaulimbiu isemayo "Miaka
25 ya EAC: Tafakari ya tulikotoka na matarajio ya tunapokwenda"