Habari
Mkutano 23 wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na Kusini (COMESA) leo tarehe 31 Oktoba 2024. Jijini Bujumbura nchini Burundi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mkutano 23 wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki na Kusini (COMESA) leo tarehe 31 Oktoba 2024. Jijini Bujumbura nchini Burundi.
Mkutano huo umelenga kuimarisha Mtengamano wa kikanda kupitia kuongeza thamani kwa kilimo himilivu kwa mabadiliko ya Tabia ya nchi na thamani ya Madini,na kuimarisha Utalii.
Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo ni moja na kuongeza fursa ya nchi ya Tanzania katika masuala ya biashara na kujenga uchumi wa nchi.