Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mkutano Maalum wa Ngazi ya Makatibu Wakuu Jumuiya ya Afrika Mashariki


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Balozi Dkt.John Simbachawene akishiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw.Elijah Mwandumbya kujadili mapendekezo ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu ufunguaji wa Soko la bidhaa (TARIFF OFFER) katika Eneo Huru la Biashara Afrika ulioanza 09-13 Septemba 2024,Jijini Arusha.

Kikao hicho cha ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kimeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi.