Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs) (katikati) akifunga Mkutano huo Novemba 07, 2024 ambapo amewahimiza kutekeleza Mkataba wa AfCFTA kwa vitendo ili kufikia malengo tarajiwa. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024.
Mkutano huo unapokea Taarifa kutoka kwa Kamati za Biashara Mtandao, Uwekezaji, Biashara ya Bidhaa, Wanawake na Vijana katika AfCFTA, Haki Bunifu na Biashara ya Huduma ili kuzijadili na kuziwasilisha katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Biashara Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 8 - 10/11/2024