Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Naibu waziri Mhe. Injinia Stella Manyanya afanya Ziara ya kutembelea kongano la ngozi na Ofisi za SIDO DODOMA.


Naibu waziri Mhe. Injinia Stella Manyanya afanya Ziara ya kutembelea kongano la ngozi na Ofisi za SIDO DODOMA. Katika ziara yake amejionea shughuli mbalimbali za wajasiliamali wadogo ambao wako chini ya SIDO, DODOMA. Mhe Naibu Waziri amewataka SIDO kuongeza ufanisi wa kiutendaji na kuwasaidia wajasiliamali wadogo ili kuweza kujiendeleza hasa kuwasaidia katika upatikanaji wa mikopo na maeneo ya kufanyia kazi.