Habari
NAIBU WAZIRI WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI ATEMBELEA CHUO CHA CBE

NAIBU WAZIRI WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI ATEMBELEA CHUO CHA CBE Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amewashauri chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuwa na utaratibu wa kuwatambua wafanyabiashara waliofanikiwa kwa kutoa ajira nyingi kwa watanzania kwa kuwapa vyeti. Naibu Waziri Mhandisi Manyanya aliyasema hayo wakati alipotembela chuo cha CBE na kuwapongeza kwa maboresho mbalimbali ambayo chuo wanayafanya ili kuboresha kiwango cha elimu chuoni hapo. Waziri alisema wakati umefika kuwatambua watu wanaofanya vizuri kwa vitendo kuthamikia kwa ubunifu wao. “Nadhani mnatikiwa kufanya utafiti ili kutambua watu waliofanikiwa ili kuwapa vyeti ikiwezekana kuwapa hata PHD ya heshima kwao kutokana na mchango wao wa kutoa ajira kwa watu wengi.” Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhandishi Manyanya amekipongeza Chuo cha CBE kwa kufanya mabadiliko makubwa yanayoendana na wakati huu. “Kwa mabadiliko haya yaliofanyika yamenifurahisha, hata mwanafunzi akikwambia anatotoka chuo cha biashara anaeleweka, tuwafundishe wanafunzi wetu wayaishi yale yanayoonekana”. Alisisitiza kuwa chuo hicho ni muhimu katika kuwabadilisha vijana kuwa na mtazamo wa namna wanavyofanya shughuli zao katika kuelekea katika uchumi wa Viwanda na pia kupata ujasiri katika kuanzisha biashara. “Natamani mitaala yetu irudi katika utendaji wa vitendo, tuwafanye vijana wetu waungane na watu wa mataifa mengine katika kuanzisha biashara” Aliwataka pia waadhiri wa chuo hicho kuwatafutia wanafunzi namna ya kukutana na wajasiliamali wadogowadogo, ili waweze kupata ujuzi na pia kuwasaidia wajasiliamali hao kupata njia bora za biashara. “Chuo kiwaandae vijana katika kuwajengea mazingira ya kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa peke yake,” alisema Naibu waziri Mhandisi Manyanya. Akimkarisha Naibu Waziri, Mkuu wa Chuo hicho Prof.Mjema alisema kwamba mbali na mafanikio waliofikia, lakini bado wanachangamoto ya kuwa na uhaba wa fedha za kujiendesha, uchakavu wa majengo chuoni hapo . “Uchache wa wafanyakazi, uvamizi wa baadhi ya maeneo ya chuo,pamoja na upungufu wa wanafunzi wanadahiliwa chuoni ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili chuo kwa sasa.