Habari
KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA DKT. HASHIL ABDALLAH AHIMIZA WANANCHI WA MANYONI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UCHAKATAJI WA KOROSHO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, amewataka wananchi wa Manyoni na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa za mafunzo na ujasiriamali zitakazotolewa kupitia Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho CAMARTEC kilichopo Masigati, Manyoni zitasaidia kuongeza kipato, kukuza ajira na kuimarisha ushindani wa soko la korosho nchini.
Akizungumza Septemba 30, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho, Dkt. Abdallah amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuliwezesha zao la korosho kupitia utafiti, pembejeo zenye punguzo na mafunzo kwa wakulima, na iko tayari kusaidia Sekta binafsi zenye nia ya kiwekeza viwanda kama hivyo.
Amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 494 kufanikisha uanzishwaji wa kiwanda hiki na kuwa mbanguaji wa korosho kwa kutumia teknolojia za kawaida ana uwezo wa kubangua kati ya kilo 20 hadi 50 kwa siku na baada ya technologies hii anaweza Kibanga kilo 40 hadi 80 kwa masaa nane, na kutoa kilo 10 hadi 20 za korosho zilizokamilika, hali ambayo inaonyesha kuwa kiwanda hicho kuwa kichocheo cha ujasiriamali na ajira.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji amesema Wilaya yake itaendelea kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na katika kuendeleza na kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara hususani katika kuendeleza Viwanda vidogo vya Kati na vikubwa ili kuongeza Ajira, Pato la Taifa na kukuza uchumi kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Camartec, Prof. Valerian Silayo,amesema kuwa kiwanda hicho cha kubangua korosho ni miongoni mwa hatua zinachukuliwa na Serikali katika kutatua changamoto kwenye kuchakata mazao ya kilimo,Mifugo,Uvuvi na Misitu.
Awali akitooa taarifa ya kiwanda hicho Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama ameeleza chimbuko la kiwanda hicho ni utafiti wa uhitaji wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini ambapo ulibaini kuwa ubanguaji wa korosho nchini,hususani kwa wakulima na wabanguaji wadogo ni changamoto.