Habari
Dkt Hashil Abdallah ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Tisa (9) wa Umoja Wa Mataifa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Tisa (9) wa Umoja Wa Mataifa kwa ajili ya kupitia taratibu na kanuni za udhibiti wa mienendo ya biashara inayokinzana na ushindani.
Akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Seleman Jafo, Dkt Abdallah ameshiriki Mkutano huo wa ngazi ya juu ambao hufanyika kila baada ya miaka 5 kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu ushindani na ulinzi wa mtumiaji katika ngazi ya kimataifa.
Mkutano huo uliowakutanisha Mawaziri, Wakuu wa Mamlaka za Ushindani, Mamlaka za Ulinzi wa Watumiaji na Maafisa Waandamizi husika kutoka nchi wanachama ulianza tarehe 07 - 11/07/2025.
Lengo la Mkutano huu ni kuchangia mageuzi yenye tija (meaningful reforms) kwenye Sera na Sheria za ushindani na ulinzi wa mlaji na kuimarisha utekelezaji wa sheria hizo katika nchi zinazoendelea.
Mkutano huo pia unatoa mwongozo kwa UNCTAD kuhusiana na program zake katika na masuala ya ushindani na ulinzi wa mtumiaji, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kiufundi na jitihada za kujenga uwezo (capacity building) kwa nchi zinazoendelea na LDCs.