Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Rais wa Uturuki awasili nchi Tanzania kwa ziara ya siku moja


Rais wa uturuki Mhe. Recep Tayyip ERDOGAN amewasili mjini Dar es salaam tarehe 22 Januari, 2017. Atakuwepo hapa kwa ziara ya kiserikali ya siku moja. Mhe. Recep anatarajia kushuhudia kusainiwa kwa mikataba mbalimbali kati ya wafanyabiashara kutoka Uturuki na wizara na taasisi mbalimbali leo tarehe 23 Januari, 2017. Leo pia atashiriki Kongamano la Biashara pamoja na mwenyeji wake Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani. Kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu (BOT) kuanzia saa nane mchana.