Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali haina mpango wa kuviua viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari kama wanavyodai baadhi ya watu.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mariam Ditopile amesema serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haina mpango wa kuviua viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari kama wanavyodai baadhi ya watu.

Ameyasema hayo kwaniaba ya Kamati iliootembelea kiwanda cha sukari cha Bagamoyo kwa lengo la kukagua shughuli za sekta binafsi zinazosimamiwa na serikali kuhakikiasha mwananchi anapata thamani ya kile anachostahiki kukipata.,Oktoba 08,2024 Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Amesema dhamira ya Rais Dkt. Samia ni kukuza viwanda hivyo kuhakikisha uzalishaji wake unaongezeka kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya sukari hususani ya viwandani ndani na nje ya nchi hivyo amewataka Watanzania kupuuza uzushi wote unaosemwa serikali inataka viwanda vya sukari nchini vife.

Aidha amesema Dkt. Samia amekuwa akiendelea na kuunga mkono juhudi za uwekezaji kwa lengo la kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya sukari hususani ya viwandani hivyo kwa hatua hizo anakwenda kufikisha nchi ya Tanzania kwenda kuuza sukari nchi jirani na mabara tofauti.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah amesema kamati imeona jinsi serikali ya Rais Dk. Samia inavyotafsiri kwa vitendo yanaliyobainisha katika miongozo mbalimbali ikiwemo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuendeleza kuendeleza sekta ya viwanda nchini ambapo muwekezaji ameridhika na sera iliyopo na kukiri hakuna changamoto isiyotekelezwa na serikali.

Dkt. Hashili ameendelea kwa kusema katika uwekezaji huo kilikuwa na changamoto ya barabara lakini inatengenezwa, bwawa la maji Wizara ya Maji imefika kushirikiana na Wizara ya Kilimo hivyo kuna mkakati wa kujenga Bwawa kubwa la maji, walisema wanachangamoto ya gati Bagamoyo, serikali imethibitisha mwezi ujao mkataba wa ujenzi wake utakamilika.