Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inatekeleza  jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji  pamoja na kutatua changamoto walizonazo.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali inatekeleza  jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji  pamoja na kutatua changamoto walizonazo.

Dkt. Kijaji amesema hayo Agosti  1, 2023 alipotembelea Kiwanda  cha Magodoro cha TANFOAM  kilichopo Jijini Arusha kujionea shughuli za uzalishaji magodoro na kisikiliza changamoto walizonazo.

Aidha, Amesema  Wizara yake inatekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambapo moja msingi yake ni kuondoa majukumu yanayofanana kati ya Taasisi ili kurahisisha ufanyaji biashara  na uwekezaji nchini

Akiongea na uongozi wa kiwanda hicho, Dkt. Kijaji amezitaka Taasisi  kuacha kufanya majukumu yanayofanana na kuzitaka kushirikiana katika kuwahudumia wafanyabiashara na wawekezaji  ili kukuza biashara na uchumi wa Taifa

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa TANFOAM Bw Mechack Jimmy ameishukuru Serikali kwa jitahada mbalimbali inazozifanya katika kutatua changamoto za Wafanyabiashara na wawekezaji ili kuwawekea mazingira bora ya ufanyaji biashara na uwekezaji.