Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Simbachawene aliongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano waTatu wa Pamoja wa Kamati ya Maafisa Waandamizi na Wataalam wa ukanda wa Kati na Mashariki mwa Afrika


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene aliongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano waTatu wa Pamoja wa Kamati ya Maafisa Waandamizi na Wataalam wa ukanda wa Kati na Mashariki mwa Afrika ulifanyika 15 - 18 Oktoba 2024, Yaoundé Cameroon.

Mkutano huo ulilenga kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika ukanda wa Kati na Mashariki mwa Afrika.

Ujumbe huo uliongozwa na Balozi Simbachawene ulijumuisha Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Dkt. Noel Komba, Mchumi Mkuu, Idara ya Sera na Bw. Muksini Mkumba, Mehumi na Afisa Dawati la UNECA, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya

Mkutano huo uliratibiwa na
Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika (United Nations
Economic Commission for Africa -
UNECA) kwa kushirikiana na Serikali ya Cameroon na ulihudhuriws na
viongozi na watalaam mbalimbali kutoka nchi wanachama nchi za ukanda wa Kati na Mashariki mwa Afrika; wawakilishi kutoka UNECA:
Jumuiya za Kikanda; Umoja wa Mataifa na taasisi zake (UN Agencies); Sekta binafsi; Asasi za kiraia; Mabaraza ya biashara (Business Councils); vyama vya wakulima, wafanyabiashara, viwanda na wajasiriamali;
watafiti; wawakilishi wa makundi ya wanawake na vijana pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo