Habari
SERIKALI NA VIETTEL (HALOTEL) WASAINI MAKUBALIANO MUHIMU YA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (Mjumbe wa timu ya Majadiliano ya Taifa - GNT) akishiriki kwenye Hafla ya kusaini Hati ya makubaliano (Deed of Settlement) na nyongeza ya Mkataba (Addendum) wa ujenzi wa Miundombinu ya Mawasiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kampuni ya Viettel Global Joint Stock (Halotel) Oktoba 06, 2025 Jijini Dodoma.