Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania na Oman kuendeleza ushirikiano wakibiashara


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amekutana na kujadiliana na Waziri wa Biashana, Viwanda na Uwekezaji wa Oman Mhe. Qais bin Mohammed Al Yousef kuhusu kuendeleza ushirikiano uliopo kwa muda mrefu katika kukuza biashara hususani katika Mazao ya Kilimo kama Kahawa, Korosho na Karafuu pamoja na Mifugo hususan nyama ya mbuzi kutoka Tanzania.

Dkt. Abdallah ameongoza ujumbe wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Abdallah katika Majadiliano hayo ya Biashara baina ya Tanzania na Oman yaliyofanyika Februari 27, 2024 sambamba na Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara wa nchi Wanachama wa WTO unaoendelea kufanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29/02/ 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa ADNEC, Abudhabi katika Falme za Kiarabu.