Habari
Tanzania na Zambia kurahisisha mazingira ya Biashara ili kuondoa vikwanzo vinavyozuia Biashara kufanyika
Tanzania na Zambia kurahisisha mazingira ya Biashara ili kuondoa vikwanzo vinavyozuia Biashara kufanyika pande zote mbili.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara wakati alipokuwa akitoa hotuba katika Mkutano wa kutiliana Saini makubaliano ya kurahisisha Biashara ndogo ndogo _Simplified Trade Regime_ (STR) uliofanyika katika Hotel ya Izukanji ilyoko Nakonde nchini Zambia.
Aidha Dkt.Simbachawene amesema bidha zilizokubaliwa katika mkataba ulisainiwa leo lazima ziwe bidhaa zinazozalishwa na nchi mwanachama ambazo zinaingia na kutoka kupitia mpaka wa Tunduma upande wa Tanzania na Nakonde upande wa Zambia.
Amezitaja baadhi ya bidhaa zilizokatika mkataba huo kuwa ni nyuzi za nguo,bidhaa za dawa,Sukari,nafaka,unga,sigara,bidhaa za kemikali,bidhaa za samani na saruji,Matunda mboga na samani,sabuni nk.
Vilevile ameeleza kuwa mkataba wa awali kuhusu urahisishaji Biashara _Simplified Trade Regime_ (STR) ulisainiwa mwaka 2017 huku ukihusisha bidhaa 22 zinazoingia na kutoka kupitia katika mpaka wa Tanzania na Zambia.
Amesema kuwa pamoja na makubaliano hayo kukubaliwa miaka 7 iliyopita kumekuwa na changamoto ya utekelezaji wake kwa kila upande wa mipaka hiyo, ndiyo maana wakaamua kukaa tena na kupitia makubaliano ya awali na kuongeza bidhaa nyingine kutoka 22 hadi kufikia 51.
Ameeleza kuwa lengo la Wizara ni kusaidia wananchi wake na kuwapunguzia kero ili kupanua wigo mkubwa wa kipato kwa wajasiamali wanaopita katika mipaka yote kwa leongo la kuongeza mitaji baade wawe wafanyabiashara wakubwa watakaofaidisha pande zote katika ulipaji kodi.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda nchini Zambia Bi. Lilian Bwalya amesema kuwa mkataba ulisainiwa leo utasaidia wafanyabiashara wadogo wa Tanzania na Zambia kupitisha bidhaa zao kwenye mpaka kwa njia halali wa Nakonde na Tunduma na kuondo wimbi la kupita njia za panya zisizo rasmi.
Ameongeza kuwa makubaliano ya mkataba ulisainiwa leo kumeongezeka bidhaa nyingine ikiwemo samaki ambao katika mkatba wa awali hawakuwemo hivyo kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Samaki kuchangamkia fursa hiyo.
"Nchi hizi mbili zinaendelea kufurahia uhusiano bora na mzuri. Tanzania na Zambia