Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA-DKT.JAFO.


WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA-DKT.JAFO.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) amewaasa Watanzania kuchangamkia fursa zinazotokea katika upande wa biashara na viwanda nchini ili kukuza uchumi.

Waziri Jafo ametoa rai hiyo wakati akifungua Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Afrika 2025 uliondaliwa na Global Chamber na Integrating Empowerment Initiative (IEI) unaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam Julai 09,2025.

Dkt.Jafo amesema ni wakati wa Watanzania kuwa mstari wa mbele katika kutumia fursa zinzopatikana nchini hasa kwa vijana na wanawake katika masomo pamoja na ushiriki wao katika masuala ya biashara.

Aidha Dkt.Jafo amesema kuwa Global Chamber kupitia Mkutano huo utasaidia kuto mafunzo ya jinsi ya kushiriki katika biashara na uwekezaji kwa Watanzania ili kuwapa uelewa mkubwa pamoja na ufadhili wa masomo kwa vijana.

Kwa uoande wake Mkurugenzi Mkuu Global Chamber and Integrating Empowerment Initiative (IEI) Bi Neema Mleli amesema kuwa Mkutano huo umeandaliwa kwa dhumuni la kujadili nafasi ya Bara la Afrika katika Biashara na uwekezaji kimataifa huku msisitizo ukiwa ni Soko Huru la Afrika (AfCFTA).

Mkutano huo umeaandaliwa na IEI, Global Chamber, Kwa kushirikiana na TradeMark Africa (TMA), Shirika la Maendeleo la Belgium (Enable)