Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

DKT.JAFO -TUNA KILA SABABU YA KUTUMIA BIDHAA ZA NDANI.


DKT.JAFO -TUNA KILA SABABU YA KUTUMIA BIDHAA ZA NDANI.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) amesema kuwa kama Watanzania kuna kila sababu ya kutumia bidhaa za ndani ili kulinda viwanda vya ndani na kutengeneza ajira kwa vijana nchini.

Amebainisha hayo wakati wa ziara yake katika Kiwanda cha kutengeneza Vioo cha Salehbhah kilichopo Jijini Dar es Salaam Julai 10,2025.

Dkt.Jafo amesema ni vizuri Watanzania kutumia bidhaa za ndani kutokana na uwezo wa viwanda vilivyopo nchini hasa kiwanda hicho kinachozalisha bidhaa mwisho za vioo (final product) katika majengo mbalimbali.

Aidha Dkt.Jafo amesema kuwa Serikali ipo pamoja na wawekezaji hao ili kuwafanya wafikie malengo yao ambayo wamejiwekea.

Vilevile Waziri Jafo amesema lengo lanziara hiyo la ziara hiyo ni kusikiliza baadhi ya changamoto na mahitaji yao katika uwekezaji wao wa Kiwanda hicho.

Nae Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bw.Mufaddal Dawaoodbhai amesema wamefarijika kwa Waziri huyo mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara kufanyabziara katika Kiwanda hicho na pia kuahidi kuendelea kuingeza uzalishaji wa bidhaa hiyo kwa manufaa ya uchumi wa Tanzania.