Habari
VIWANDA VITATU VILIVYOSIMAMA UZALISHAJI VYAFUFULIWA MKOA WA TANGA
Viwanda vitatu (3)vilivyosimama uzalishaji kwa sababu mbalimbali vimefufuliwa na vitaanza uzalishaji kamili Januari 2026 baada ya kukamilisha hatua mbalimbali ikiwemo ufungaji wa mitambo katika kipindi cha majaribio ya uzalishaji, Mwezi Disemba 2025.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Oktoba 13, 2025 akiwa ameambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Rashid Mchatta pamoja na Wataamu wa Serikali wakati wa Ziara katika viwanda hivyo Jijini Tanga kwa lengo la kuangalia utekelezi wa jitihada mbali zinazoendelea katika kufufua Viwanda Mkoani humo ili kuifanya kuwa Tanga ya Viwanda.
Aidha, Dkt Abdallah ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Sera, Miongozo na kuwezesha ufufuaji wa Viwanda hivyo ambavyo vitaongeza ajira , Pato la Taifa pamoja na uchumi kwa ujumla.
Viwanda vilivyotembelewa katika ziara hiyo ni Kiwanda cha Unique Steel Rolling kinachozalisha bidhaa za Chuma, Kiwanda cha Ply and Panel kinachotengeneza bidhaa za Mbao ikiwemo samani na magogo pamoja na Kiwanda cha African Harmony kinachozalisha bidhaa za Sabuni Amesema Dkt Abdallah.
Naye, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Rashid Mchatta ameahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuhakikisha Mkoa wa Tanga wenye raslimali nyingi yakiwemo madini pamoja na Bandari unakuwa na viwanda vingi vinavyofanya kazi ili kukuza uchumi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kiwanda Ply&Panel Limited na Unique Steel Rolling Bw. Hussein Moor pamoja na Meneja Raslimali Watu wa Bw African Harmony Bw. Ahmed Mtomola wameishukuru Serikali kwa kuwezesha ufufuaji wa viwanda hivyo na kuahidi Kuwa viwanda hivyo vitatoa ajira kwa watu wengi vitakapoanza kizalisha kikamifu.
Nao Wafanyakazi katika Kiwanda cha African Harmony Bw. Edward Mnzava na Richard Mkama wamesema wamefurhishwa na hatua ya Serikali kuwezesha ufufuaji wa Viwanda hivyo vinavyotoa ajira za moj kwa moja na zisizo za moja kwa moj kwa Vijana wa Mkoa huo ambayo wengi walikuwa Mtaani kwa kukosa ajira.
