Habari
Ujumbe kutoka Serikali ya China Idara ya Biashara yaja na fursa Tanzania

UJUMBE KUTOKA SERIKALI YA CHINA IDARA YA BIASHARA YAJA NA FURSA TANZANIA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade ) Bi Latifa M. Khamis amepokea ujumbe kutoka Idara ya Biashara “Department of Commerce kutoka Serikali ya China yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya serikali zote mbili, ugeni huu umepokelewa leo tarehe 21 Februari, 2025 katika ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl JK Nyerere, barabara ya Kilwa Jijini Dar es salam.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha kushiriki katika Kongamano la “Lake Tanganyika Business Forum” ambalo litafanyika katika Mkoa wa Kigoma, pamoja na kushiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam maarufu kama “Sabasaba“ ya mwaka 2025.
@ikulu_mawasiliano @samia_suluhu_hassan @temeke_mc @brela_tanzania @viwandabiashara @brela_tanzania @sido @samia_suluhu_hassan @dr_philip_isdor_mpango @kassim_m_majaliwa @biteko @owm_tz @ofisi_ya_makamu_wa_rais @jerrysilaa @wizarahmth @ikulu_mawasiliano @msemajimkuuwaserikali @albert_john_chalamila @sixtusmapunda @jomaarysatura @mkubwafellatmk @daressalaam_rs_digital @mkengajumarajabu @abbasmtemvu @mhe_mariammtemvu @lwizafulgence @selemani_jafo @viwandabiashara @tbc_online @tbctaifa @tbctaifa @efmtanzania @etvtanzania @efmtanzania @basata.tanzania cloudsfmtz @tcra_tanzania @gersonmsigwa @yangasc @simbasctanzania