Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara kukataa vitendo vya rushwa, kubadilika na kufuata maadili ya utumishi wa umma katika utendaji kazi wao wa kila siku na utoaji huduma kwa umma.


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Sempeho Manongi ametoa rai kwa Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara kukataa vitendo vya rushwa, kubadilika na kufuata maadili ya utumishi wa umma katika utendaji kazi wao wa kila siku na utoaji huduma kwa umma.

Vile vile Bw. Manongi ameshauri kuwa semina za maadili na rushwa zifanyike mara kwa mara kwa watumishi wa wizara hiyo ili Kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma kwa kufuata maadili, weledi, uadilifu na uaminifu ili kutimiza malego ya wizara iliyojiwekea katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara nchini.

Bw. Manongi ameyasema hayo Disemba 06, 2024 wakati wa Semina ya Maadili na Rushwa kwa Watumishi wa Wizara hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji, Mtumba Dodoma.

Aidha Bw. Manongi amebainisha kuwa Semina ya Maadili na Rushwa kwa watumshi wa Wizara hiyo ni utekelezaji wa Mpango Kazi wa Idara ya Utawala na Raslimali watu kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya Wizara katika mwaka wa fedha 2024/2025,

Bw. Manongi pia amesema kuwa semina hiyo muhimu ilihusisha watoa mada kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Nao watoa mada hao kwa nyakati Tofauti wa waliwaelimisha na kuwakumbusha watumishi hao kufuata maadili katika utendaji kazi wao kwa ujumla pamoja na kukataa kutenda vitendo vya rushwa ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma kwa kuwa Sekta ya Viwanda na Biashara ni moja ya sekta muhimu katika kukuza biashara na uchumi wa nchi kwa ujumla.