Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri Mwijage Akutana na Mshindi wa Tuzo Ya ‘African Entreprenureship Award’


Waziri Mwijage Akutana na Mshindi wa Tuzo Ya ‘African Entreprenureship Award’ Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage leo amekutana na kuwa na mazungumzo na mshindi wa Tuzo ya ‘African Entreprenureship Award’, Bi. Jennifer Shigoli ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Malkia Investment iliyobuni na ina mpango wa kuzalisha taulo za kike ziitazo ELEA. Katika mazungumzo hayo Mhe.Mwijage alimpongeza mjasiliamari huyo kwa kuweza kufanikiwa kupata tuzo hiyo ambayo imeliletea Taifa sifa na alimtaka kuongeza juhudi katika shughuli zake. Aidha Mhe.Waziri amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO) pamoja na Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CARMATEC)kuwasaidia na kuwaendeleza Wajasiliamari wadogo ili waweze kusonga mbele. “waonyeshe wafanye nini ili wafanikiwe, msipoteze muda kuwaambia sharia inazuia nini” alisema Mwijage. Kwa upande wake Bi. Jennifer alimshukuru Mhe. Waziri kwa kuonyesha nia yakuwasaidia wajasiliamali na amehaidi kuongeza jitihada katika shughuli zake ili kuiwezesha jumuiya ya Watanzania kupata ufumbuzi wa tatizo la taulo za kike kwa Wanawake wa Tanzania. Kampuni ya Malkia Investment ni kampuni ya binti wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 26 ambaye amebuni taulo za kike zitakazokidhi matakwa ya soko. Taulo hizo zinatarajiwa kuwa za bei nafuu kwa kila mtu kumudu kwani zinaweza kutumika zaidi ya mara moja na ni safi na salama.