Habari
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akutana na waandishi wa habari Leo jijini DSM.
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 27/7/2017. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akutana na waandishi wa habari na kuzungumza nao juu ya hatma ya Viwanda vilivyobinafsishwa. Mhe Waziri ameyasema hayo leo jijijini DSM kwa kuwaeleza waandishi juu ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha Viwanda vyote ambavyo havifanyi kazi vinaanza kufanya kazi mara moja. Mhe. Waziri ameunda kamati itakayo shirikisha wataalamu kutoka idara za serikali na wakuu wa mikoa yote Tanzania, kuvitembelea na kuvikagua na kutoa taarifa ya maamuzi kwa viwanda vitakavyokuwa havifanyi kazi kwa kutokutii agizo la mhe. Rais alilolitoa mkoani Pwani katika ziara yake ya kutembelea na kuzindua viwanda.