Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali itahakikisha inakisaidia Kiwanda cha kutengeneza Vipuri Kilimanjaro ( KMTC)

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali itahakikisha inakisaidia Kiwanda cha kutengeneza Vipuri Kilimanjaro ( KMTC) kufikia malengo katika masoko kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuona uzalishaji wa ndani unafanyika kupitia chuma kinachozalishwa nchini.
Amesema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro kujionea shuhhulizilipo pamoja na kisikiliza na kitatua changamoto zao.
Aidha amewapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho n kiwataka kuwa waaminifu kwa kiwa Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuweka mazingira bora ya biashara ili kuvutia wawekezaji katika viwanda vitakavyotumia vipuri vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.