Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali  ya Awamu ya Sita haiko tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali  ya Awamu ya Sita haiko tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao bali itawasaidia  kukua na kuendelea kibiashara, kukaa kwa pamoja  na kutatua changamoto zao ili kuhakikisha ufanyaji biashara wao unakuwa na tija na manufaa kwa Taifa .

Amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vishikwambi cha Tanztech kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea uzalishaji huo na kusikiliza  changamoto zao. 

Aidha Dkt. Kijaji amesema ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia TEHAMA  katika mitaala ya elimu